Pata taarifa kuu
BURUNDI-RED TABARA-USALAMA

Waasi kumi na nne wauawa katika mapigano Magharibi mwa Burundi

Polisi ya Burundi imetangaza kwamba imeua wapiganaji kumi na nne na kukamata wengine wengi, bunduki 11 na vifaa vingine vya kijeshi katika mapigano yaliyotokea wilayani Musigati katika mkoa wa Bubanza Magharibi mwa Burundi, kilomita zaidi ya 15 na mpaka na DRC.

Maafisa wa polisi wakipiga doria katika wilaya ya Ngagara, Bujumbura Aprili 27, 2015.
Maafisa wa polisi wakipiga doria katika wilaya ya Ngagara, Bujumbura Aprili 27, 2015. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Mapigano kati ya vikosi vya usalama na ulinzi dhidi ya kundi la wapiganaji yalianza mapema asubuhi Jumanne wiki hii katika mkoa wa Bubanza. Lakini taarifa hiyo ya mapigano haikuweza kutolewa papo hapo, kulingana na kile jeshi limesema lilikuwa likisubiri kutokomeza kundi hilo.

Hata hivyo taarifa ya mapigano hayo iliendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Facebook, Twitter na hasa Whatsapp, huku raia wakichukuliwa kama uvumi tu.

Kwa mujibu wa mashahidi hayo ya kwanza kutokea tangu mwanzon mwa mwaka huu, yalidumu saa 13, na pande zote zimepoteza.

Wapiganaji wengi walionekana katika Wilaya za Mpanda, Gihanga na eneo la Mitakataka, mkoani Bubanza tangu mwishomi mwa wiki iliyopita wakijaribu kuingia katika Msitu wa Kibira baada ya kuvuka Mto Rusizi unaotenganisha DRC na Burundi, kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi ambavyo havikutaja majina.

Kundi la waasi la Red-Tabara limekiri kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa wapiganaji wake ndio walikabiliana vikali na vikosi vya usalama na ulinzi vya Burundi katika mapigano yaliyotokea Jumanne mchana wiki hii na kwamba wanaendelea kuingia nchini Burundi kwa lengo la kurejesha utawala wa sheria nchini Burundi.

Vyanzo kadhaa vya polisi ambavyo havikutaja majani vimebaini kwamba makundi ya waasi wa Burundi, Red-Tabara, FNL na Forebu yameweka ngome zao mashariki mwa DRC, kwa lengo la kuingia kuirahisi nchini Burundi kuanzisha vita dhidi ya utawala uliopo sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.