rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania Kenya Uganda Rwanda

Imechapishwa • Imehaririwa

Mamlaka za hali ya hewa zaonya uwepo wa mvua kubwa Afrika mashariki

media

Mamlaka za utabiri wa hali ya hewa katika nchi za Afrika Mashariki, hasa nchini Kenya, Rwanda na Tanzania, zinaonya kuwa mbua kubwa zitaendelea kunyesha hadi mapema mwaka ujao, wakati huu maafa na madhara yakiripotiwa.


Mvuo hizo zimekuwa zimekuwa zikinyesha kwa kipindi cha wiki moja sasa na kusababisha maafa.

Nchini Tanzania watu 29 wamepoteza maisha katika mikoa ya Tanga na Morogoro, huku Kenya ikishuhudia vifo vya watu wanane.

Mamlaka katika nchi hizo za Afrika Mashariki, zinasema kuwa mvua zitaendelea kushuhiwa gadi mapema mwezi Februari mwaka 2020.

Iwapo hali hiyo itaendelea kushuhudiwa, basi huenda vifo zaidi vikashuhudiwa lakini pia mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu.

Mataifa ya Afrika Mashariki, huwa yanashuhudia kipindi kifupi cha mvua kati ya mwezi Oktoba na Novemba.

Hali mbaya ya miundo mbinu katika nchi hizo zimeendelea kusababisha mafuriko makubwa wakati mvua zinaposhuhudiwa.