rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Al Shabab

Imechapishwa • Imehaririwa

Polisi ya Kenya yaimarisha usalama Kaunti ya Mandera

media
Kikosi cha Ulinzi cha Kenya baada ya shambulio la wanamgambo wa Al Shabab katika Chuo Kikuu cha Garissa Aprili 2015. CARL DE SOUZA / AFP

Polisi katika Kaunti ya Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya wapo katika hali ya tahadhari, baada ya kuripotiwa kuwa washukiwa 20 wa Al Shabab kutoka nchini Somalia walikuwa wameonekana katika eneo hilo.


Ripoti zinasema kuwa, magaidi hao walionekana katika maeneo ya Bale-Ilman Mala na Kutulo Ijumaa iliyopita.

Haya yanajiri wakati huu miili ya maafisa 11 wa polisi waliouawa Jumamosi iliyopita huko Garissa wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi kilichotegwa ardhini ikirejeshwa jijini Nairobi.

Kenya imeendelea kuwa kwenye vita na kundi la Al Shabab tangu mwaka 2011, ilipotuma wanajeshi wake nchini humo.