rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Maandamano nchini Iraq: Takwimu rasmi za watu waliouawa ni 157, pamoja na 111 Baghdad
  • Machafuko Chile: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 15 baada ya watu watatu kuuawa (serikali)

Sudani Kusini Salva Kiir Riek Machar

Imechapishwa • Imehaririwa

Riek Machar asogeza mbeke kurudi kwake Sudani Kusini mbele kwa muda usiojulikana

media
Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar. © ASHRAF SHAZLY / AFP

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini anatarajiwa kurudi Juba Novemba 12 kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Walakini, utekelezaji wa mkataba wa amani wa Septemba 2018 umechelewa kwa muda mrefu. Kambi ya Riek Machar inashutumu serikali kutaka kukwamisha mchakato wa amani.


Sintofahamu imeibuka siku chache kabla ya tarehe 12 Novemba, tarehe ambayo kiongozi wa waasi Riek Machar anatarajiwa kurudi Juba. Chama cha SPLM-IO cha Riek Machar, kimetoa orodha ya mambo ambayo huenda yakakwamisha zoezi la kurudi kiongozi wao Juba: hali ya usalama haitoshi, zoezi la kuundwa kwa jeshi la umoja limecheleweshwa sana na suala la kugawana madaraka katika majimbo halijatatuliwa. Kutokana na hali hiyo, chama cha Riek Machar kimetangaza kwamba "hakitashiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa".

Kambi husika katika mkataba huo zilipaswa kuunda kikosi cha kwanza cha askari 83,000, ambapo nusu ya kikosi hicho ilitarajiwa kuwa tayari mnamo mwezi Novemba, na pia kundi la watu 3,000 kutoka kambi zote mbili kulinda viongozi wa serikali. Walakini, mchakato huu tayari umechelewa kwa muda mrefu. "Haiwezekani kutoa mafunzo kwa jeshi kwa mwezi mmoja. Serikali ilisitisha mchakato huo kwa kukataa kutoa fedha, "chama cha SPLM-IO cha Riek Machar kimeshtumu.

Kuhusu suala la majimbo, Rais Kiir anatuhumiwa kwa kutaka kudhibiti mipaka ya jadi kwa niaba ya kabila lake la Dinka. Tume zilitarajiwa kujadili suala hilo, lakini kazi hiyo ilizuiliwa. Kwa mujibu wa Alfred Youhanis Magok, mmoja wa wasemaji wa Riek Machar, suluhisho zinahitajika kabla ya kiongozi wa waasi kurudi. "Mnamo mwaka wa 2016, ilifikiriwa kuwa kila kitu kitarekebishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri. Lakini serikali haikutaka kushirikiana na wengine kwa kutatua suala hilo. Hali hiyo inajirudi, "anasema Youhanis Magok.

Mtafiti Lauren Blanchard anasema hashangazwi na hali hiyo. Kwa mujibu wa mtafiti huyo, "dhamira ya kisiasa ni dhaifu, hali ya usalama haitoshi na watu hawana imani na kauli za viongozi serikalini".