Pata taarifa kuu
UKARA-MV Nyerere-TANZANIA

Ukara, kisiwa kilichohifadhi mkasa wa MV Nyerere

Alhamisi ya Septemba 20 mwaka 2019 ni siku isiyosahaulika miongoni mwa wakazi wa kisiwa cha Ukara. Kisiwa hiki na Tanzania kwa ujumla ilikumbwa na mkasa wa kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere. 

Mnara wa kumbukumbu katika eneo walilozikwa wahanga wa Mkasa wa MV Nyerere
Mnara wa kumbukumbu katika eneo walilozikwa wahanga wa Mkasa wa MV Nyerere RFI/Fredrick Nwaka
Matangazo ya kibiashara

Kivuko hicho kikiwa na makumi ya abiria kilizama pemezoni mwa mwalo wa Bwisya, kilikuwa kikifanya safari kutoka Bugorola hadi Ukara, safari ambayo huchukua saa moja.

Nyuso za wakazi wa kisiwa hiki zingali na majonzi na baadhi ya wakazi wanasema mkasa huo ungali unawasumbua kisaikolojia.

Nilifika kisiwani hapa asubbuhi ya Septemba 20, mwaka 2020 nikiwa katika ziara ya kikazi, kwa hakika ni eneo gumu kufikika kijiografia kutokana Mwanza.

Eneo la Bwisyia kulikotokea mkasa wa kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere- 20/9/2019
Eneo la Bwisyia kulikotokea mkasa wa kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere- 20/9/2019 RFI/Fredrick Nwaka

Siku hiyo kulifanyika misa ya kumbukumbu kwa wahanga wa mkasa ambapo miili tisa kati ya 226 imezikwa eneo hilo na kuwekwa mnara wa kumbukumbu.

Wakazi wa upande wa Bugorola na wale wa Ukara walinieleza wazi kuwa wangali na kumbukumbu za mkasa huo ambao ulisababisha vifo vya watu 226.

“Nilipoteza kaka yangu nami nilinusurika kwa sababu nilichelewa safari kutoka mnadani hapa Bugorola,”anasema Magori Nyeika, mkazi wa Ukara niliyesafiri naye kwenye kivuko cha MV Ukara kutoka Bugorola hadi Ukara.

Mwanahabari wa RFI Kiswahili Fredrick Nwaka, alipotembelea eneo la Bwisya walikozikwa wahanga wa MV Nyerere. 20/9/ 2019
Mwanahabari wa RFI Kiswahili Fredrick Nwaka, alipotembelea eneo la Bwisya walikozikwa wahanga wa MV Nyerere. 20/9/ 2019 RFI

Hata hivyo bado kuna changamoto ya usafirishaji kwa sababu MV Ukara na MV Sabasaba ambazo zinafanya safari lakini wingi wa abiria umekuwa ni changamoto.

Afisa wa serikali kisiwani Ukara, James Peter anasema serikali imeahidi kuimarisha shughuli za usafiri huku kukiwa na mpango wa kununua kivuko kipya kitakachokidhi idadi ya wananchi

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.