rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Rwanda Uganda EAC

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu nane wauawa Kaskazini mwa Rwanda baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha

media
Wilaya ya Musanze nchini Rwanda Thomas Mukoya/Reuters

Watu wasiojulikana wenye silaha wametekeleza mauaji ya watu nane na kuwajeruhi wengine 18 usiku wa kuamkia Jumamosi, Kaskazini mwa nchi ya Rwanda.

 


Tangazo kutoka  jeshi la polisi nchini humo,  linasema tukio la mauaji hayo lilitokea  katika tarafa za Kinigi na Musanze wilayani Musanze jimbo la Kaskazini mwa nchi hiyo.

Aidha, taarifa hizo zimeeleza kuwa watu wasiojulikana ndio waliotekeleza mauaji hayo katika kijiji cha Kaguhu tarafa ya Kinigi lakini pia yametekelezwa kwa wakati mmoja katika kijiji kingine cha Mufukuru kata ya Kabazungu tarafa ya Musanza.

Imebainika kuwa silaha zilizotumika katika kutekeleza mauaji hayo ni bunduki pamoja na zile za jadi.

Kwa mujibu wa shuhuda mmoja ameviambia vyombo vya habari Kaskazini mwa nchi hiyo ni  kuwa, katika familia moja wauaji hao waliwauwa  baba mmoja na vijana wake wawili.

Huu ni uvamizi wa tatu kufanywa katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo mauaji ya awali yalifanywa katika vijiji vilivyo karibu na pori la Nyungwe kati ya Rwanda na Burundi.

Ripoti ya Mwandishi wetu wa Kigali, Bonaventure Chubahiro.