Pata taarifa kuu
EBOLA-TANZANIA-MAREKANI-DRC-WHO

Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake wanaokwenda nchini Tanzania

Marekani imetoa tahadhari kwa raia wake wanaokwenda nchini Tanzania, wakiwataka wajihadhari kutokana na ripoti zinazodai kuwa huenda kuna maambukizi ya Ebola katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Watalaam wa afya wanaopambana na Ebola Mashariki mwa DRC
Watalaam wa afya wanaopambana na Ebola Mashariki mwa DRC REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja, baada ya hivi karibuni Shirika la afya duniani WHO kusema kuwa Tanzania ilikuwa haitoi taarifa za kutosha kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa ugonjwa huo.

Hata hivyo serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya afya imesema, hakuna maambukizi ya Ebola nchini humo na hakuna mgonjwa yeyote aliyeonesha dalili za kuambukziwa  na kuwataka raia wake kutokuwa na hofu.

Mataifa ya Afrika Mashariki yameendelea kuwa katika hali ya tahadhari kutokana na maambukizi ya Ebola Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kusababisha zaidi ya watu 2,100 kupoteza maisha.

Tanzania inapakana na DRC lakini imegawaywa na Ziwa Tanganyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.