Pata taarifa kuu
RWANDA-FDU-USALAMA

Wauaji wa mwanasiasa wa upinzani Rwanda wakamatwa

Polisi nchini Rwanda wamewakamata watu wawili kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini humo Syridio Dusabumuremyi wa chama cha FDU.

Victoire Ingabire Umuhoza, kiongozi wa chama cha FDU, Aprili 7, 2010.
Victoire Ingabire Umuhoza, kiongozi wa chama cha FDU, Aprili 7, 2010. AFP/Bertrand Guay
Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini Rwanda wamethibitisha kuuawa kwa Syridio Dusabumuremyi jana usiku baada ya kushambuliwa kwa kisu na watu wawili waliomvamia tukio ambalo chama chake kinalihusisha na siasa.

Awalii Idara ya upelelezi nchini Rwanda ilituma ujumbe katika mtandao wa twitter kueleza kwamba imewakamata washukiwa wawili wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya Syridio Dusabumuremyi.

Kiongozi wa chama cha FDU, Victoire Ingabire amedai kuwa wanasiasa wa chama chake wamekuwa wakilengwa na kuuawa kwa sababu za kisiasa huku Rwanda ikikabiliwa vitendo vya utekaji na mauaji vya wanasiasa.

Syridio Dusabumuremyi, mratibu wa chama hicho cha upinzani FDU-Inkingi, alikuwa kazini wakati aliposhambuliwa na wanaume wawili, kwa mujibu wa kiongozi wa chama hicho Victoire Ingabire

Wapinzani wanne kutoka chma cha FDU wameuawa na wengine hawajulikani walipo. Serikali ya Rwanda inanyooshewa kidolea cha lawama kwa visa hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.