rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Burundi

Imechapishwa • Imehaririwa

Warundi waendelea kutoroka nchi na kukimbilia DRC

media
Wakimbizi wa Burundi katika kambi ya Gashora, Bugesera, Mei 9, 2015. AFP / St├ęphanie AGLIETTI

Katika siku za hivi karibuni, kambi za muda za wakimbizi katika maeneo ya Sange na Kavimvira, mashariki mwa DRC zimeendelea kupokea wakimbizi kutoka Burundi.


Zaidi ya watu 100 wanaripotiwa kuvuka mpaka kwa siku na kuorodheshwa katika kambi hizo. Hali hiyo ilianza wiki mbili zilizopita, kwa mujibu wa Gazeti la Burundi la Iwacu. Wakati wanaendelea kusubiri msaada, wakimbizi hao wanaishi katika mazingira mabaya, baadhi wanaonekana mitaani wakiomba omba.

Katika kambi ya muda ya wakimbizi ya Sange, iliyoko kilomita 15 kutoka Mto Rusizi, kwenye mpaka wa Burundi na DRC, watu wengi wamekuwa wakitoroka makaazi yao upande wa wilaya ya Buganda katika mkoa wa Cibitoke, magharibi mwa Burundi, wakijielekeza katika kambi hiyo, inayopatikana katika Jimbo la Uvira.

Kwa mujibu wa gazeti la Iwacu, ili kupata chakula cha kutosha, wakimbizi hawa, watu wazima na watoto wamekuwa wakiranda randa mitaani wakiomba omba kwa kusubiri misaada ya kibinadamu. Kwa mujibu wa mkaazi mmoja wa Sange, akinukuliwa na gazeti la Iwacu, watoto huingia nyumba kwa nyumba wakiomba msaada.

Wakati huo huo serikali ya Tanzania hivi karibuni ilitangaza kwamba itachukuwa hatua ya kuwarudisha makwao wakimbizi wa Burundi waliokimbilia nchini Tanzania.

Hayo yanajiri wakati Serikali ya Rwanda imetangaza kuwapa bima ya afya wakimbi kutoka Burundi waliokimbia nchini humo tangu mwaka 2015 kutokana na mzozo wa kisiasa na kiusalama nchini mwao.

Tangu mwaka 2017 Rwanda inatoa hifadhi kwa wakimbizi 172,000 huku asilimia 50 wakitokea nchini Burundi na wamepewa hifadhi katika kambi ya Mahama.