rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Rwanda Benki ya Dunia WB

Imechapishwa • Imehaririwa

Financial Times: Rwanda haijafikia kupunguza umaskini

media
Mtoto ombaomba katika moja ya maeneo mjini Kigali, Rwanda. (Picha ya kumbukumbu) © JOSE CENDON / AFP

Gazeti la kila siku la Uingereza la Financial Times limethibitisha makosa kuhusu takwimu za umaskini nchini Rwanda. Benki ya Dunia ilitahadharishwa mnamo mwaka 2015 na wafanyakazi wake kadhaa kuhusu udanganyifu huo, kwa mujibu wa Fincial Times.


Uchumi wa miujiza wa Rwanda umekuwa ukihojiwa mara kadhaa na wasomi, hasa mnamo mwaka 2015 baada ya kuchapishwa takwimu zilizoonyesha kupunguka kwa kiwango cha umaskini kwa alama sita kati ya mwaka 2011 na 2014.

Ni katika kipindi hicho ambapo waandishi wa habari wawili kutoka Financial Times walifanya uchunguzi.

Kwa upande wa Financial Times, kiwango cha umaskini hakikupungua kati ya mwaka 2011 na 2014. Badala yake, kiliongezeka. Kwa mujibu wa maafisa waliofanya uchunguzi huo, bei iliongezeka zaidi, hasa katika maeneo ya vijijini. Lakini mfumuko mkubwa wa bei pia unamaanisha umaskini mkubwa, imebaini Financial Times.

Hata washauri wanaoshirikiana na Rwanda wametoa takwimu zinazotofautiana sana na data za serikali, gazeti hilo la Uingereza limehakikisha, huku likitoa ushahidi.

Ndani ya Benki ya Dunia, suala hili pia limeleta mgawanyiko. Mnamo mwezi Desemba 2015, wafanyakazi watano wa benki hiyo walitoa tahadhari kuhusu kuongezeka kwa umasikini nchini Rwanda.

Hata hivyo Benki ya Dunia, tangu mwaka 2015 imekuwa ikitetea tathmini ya serikali ya Rwanda.

Rwanda, kwa upande wake, imefutilia mbali ripoti hiyo ya uchunguzi wa gazeti la kila siku la Uingereza la Financial Times. Kwa mujibu wa serijkali ya Rwanda, maendeleo yaliyopatikana katika kupunguza umasikini hayawezi kubatilishwa.