rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania

Imechapishwa • Imehaririwa

Polisi ya Tanzania yakana 'kumteka' mwanahabari Erick Kabendera

media
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akizungumza na wanahabari leo Julai 30 mwaka 2019 Jijini Dar es salaam, Tanzania RFI Kiswahili/Fredrick Nwaka

Polisi ya Tanzania imekana kumteka mwanahabari Erick Kabendera na kuainisha kwamba mwandishi huyo wa habari anashikiliwa na vyombo vya usalama na anahojiwa kuhusu uhalali wa uraia wake.


Kamanda Wa Kanda Maalumu Lazaro Mambosasa anasema Polisi ilimpa wito Wa kumwita kwa Mahojiano lakini Hakufika.

"Huyu mtu hajatekwa, anashikiliwa na yupo kituoni Hapa, tunachunguza Uraia wake kwa kushirikiana na uhamiaji,"

Hata Hivyo Mambosasa hajaeleza kwa kina kwa nini jeshi hilo linachunguza uraia Wa Mwanahabari huyo na Kusema akisema huenda akaharibu uchunguzi.

Amewataka Watanzania kuepuka Habari zinazoweza kuzua taharuki.

Erick Kabendera amewahi kuandikia magazeti kadhaa ya ndani na nje ya Tanzania na ni mmoja wa wanahabari  wanaoheshimika kwa kazi zao.