rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Bobi Wine Yoweri Museveni

Imechapishwa • Imehaririwa

Uganda: Bobi Wine ajitangaza kuwa mgombea urais mwaka 2021

media
Bobi Wine, Septemba 24, 2018, Kampala. FILE PHOTO: Ugandan musician turned politician, Robert Kyagulany

Mwanamuziki nguli na wa mbenge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi, almaarufu Bobi Wine, ametangaza leo Jumatano nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2021. Mbunge huu ni mwiba kwa rais Yoweri Kaguta Museveni.


"Kwa niaba ya raia wa Uganda, nitakabiliana na wewe (Yoweri Museveni) katika uchaguzi huru na wa haki mnamo mwaka 2021," amesema mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye ni mpinzani mkuu wa rais Museveni.

Yoweri Museveni, anatawala nchi ya Uganda tangu mwaka 1986.

Katika miezi ya hivi karibuni, mamlaka imekuwa ikimzuia mara kwa mara kuonekana hadharani.

Bobi Wine alikamatwa mara kadhaa, na kushitakiwa kwa tuhuma za uhaini, lakini Mahakama ya Kijeshi Nchini Uganda ilimwondolea mashtaka.

Hivi karibuni Bobi Wine alipigwa marufuku kufanya tamasha la muziki, utawala ukisema una taarifa kwamba kuna watu walioandaliwa kuhatarisha usalama.