rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania John Pombe Magufuli

Imechapishwa • Imehaririwa

ATCL kuanza safari za kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini

media
Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ATCL, ikiwa kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Swahili Hub

Shirika la ndege la Tanzania kesho Juni 28 mwaka 2019 litaanza safari za kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini.


Hii ni mara ya kwanza kwa shirika kuanza safari hizo tangu lilipoanza mkakati wa kujipanua kibiashara kwa safari za ndani na nje ya Tanzania.

Mkurugenzi mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladslaus Matindi ameiambia RFI Kiswhaili kwa njia ya simu kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kibiashara wa muda mrefu wa shirika hilo.

"Mkakati ni kujiimarisha kwa sababu tunajua tuna uwezo wa kushindana katika njia hizo tunazoendelea kuingia. Tunarudi katika maeneo tuliyokuwa tunatoa huduma,"amesema Matindi

Hata hivyo licha ya uwepo wa mashirika mengi ya ndege kama Kenya Airways, RwandAir na Ethiopia Airways yanayofanya safari nchini humo Matindi anasema haitakuwa changamoto kwa ATCL kwa kuwa imejipanga kutoa huduma ya uhakika kwa wasafiri na amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kutumia shirika hilo.

Shrika la ndege la Tanzania limefufuliwa na serikali ya rais John Magufuli iliyoingia madarakani mwaka 2015.