Pata taarifa kuu
UGANDA-EAC-HAKI-SIASA

Uganda: Mahakama ya EAC haina mamlaka ya kutoa uamuzi kuhusu kipengele cha umri wa rais

Serikali ya Uganda inasema kuwa mahakama ya Afrika Mashariki iliyoko mjini Arusha nchini Tanzania, haina mamlaka ya kusikiliza kesi kuhusu kipengele cha umri wa rais.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni  anatarajia kuwania katika uchaguzi wa urais ujao.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni anatarajia kuwania katika uchaguzi wa urais ujao. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii ilipelekwa kwenye mahakama hiyo na wanaharakati wakitaka ibatilishe uamuzi wa mahakama ya katiba iliyokubaliana na bunge kuondolewa kwa ukomo wa umri wa mtu kuwania urais mwezi Aprili mwaka huu.

Serikali ya Uganda ilikuwa ikijibu kesi iliyowasilishwa mbele ya majaji wa mahakama hiyo ambao watatoa uamuzi ikiwa wanaweza kusikiliza kesi hiyo au la.

Pendekezo la kuondoa ukomo kwa mgombea urais Uganda lilowasilishwa bungeni limesababisha mvutano mkubwa uliopelekea uvunjifu wa amani ndani ya Bunge.

Hatua ya kuondoa kiwango cha umri ilionekana kama juhudi za Museveni kuongeza utawala wake. Wakosoaji wake wanasema Museveni anataka aongoze taifa hilo hadi kifo kitakapomkuta.

Uchaguzi ujao nchini Uganda utafanyika mwaka 2021 kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, na umri wa mwisho wa kugombea urais kabla ya Katiba kufanyiwa marekemisho ulikuwa miaka 75. Rais Museveni atakuwa na umri wa miaka 76 wakati wa Uchaguzi huo.

Rais Yoweri Museveni ambaye ana umri wa miaka 75, ametawala Uganda tangu alipochukua madaraka kwa nguvu mwaka 1986.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.