rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Somalia Al Shabab Ugaidi

Imechapishwa • Imehaririwa

Mahakama nchini Kenya kuwahukumu washtakiwa wanne wa ugaidi

media
Washukiwa wanne wa shambulizi la kigaidi nchini Kenya, wanaotuhumiwa kuhusika na shambulizi la Chuo Kikuu cha Garissa mwaka 2015 â„¢dailyactive

Mahakama nchini Kenya inatarajia kutoa hukumu kwa washtakiwa wanne, waliotuhumiwa kuhusika na shambulizi la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garrisa mwezi Aprili mwaka 2015 na kusababisha vifo vya watu karibu 150, wengi wakiwa ni wanafunzi.


Wanne hao ni pamoja na raia wa Tanzania Rashid Mberesero, Sahal Diriy Hussein, Hassan Edin Hassan na Muhamed Abdi Abikar.

Wakati kesi hiyo ikiendelea, washtakiwa wote walikanusha mashtaka 156, likiwemo lile la ugaidi.

Kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka nchini Somalia, lilijigamba kuhusika na shambulizi hilo baya katika chuo hicho ambacho kinapakana karibu na mpaka wa Somalia.

Magaidi hao walivamia Chuo hicho wakati wanafunzi wakiwa kwenye sala ya alfajiri na kuwateka wanafunzi hao Wakiristo kwa Waislamu kwa saa zaidi ya 15 kabla ya operesheni hiyo kumalizika.