Pata taarifa kuu
KENYA-EBOLA-DRC-UGANDA

Mgonjwa mwenye dalili za Ebola atibiwa Kenya

Mwanamke mmoja anatabiwa katika Hospitali ya Kaunti ya Kericho, Magharibi mwa Kenya baada ya kuonekana na dalili za ugonjwa hatari za Ebola.

Watalaam wa Ebola
Watalaam wa Ebola afro.who.int/photo
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, mwanamke huyo alikuwa ametokea katika mpaka wa Kenya na Uganda wa Malaba na alikuwa mjini Kericho, kumsalimu mume wake.

Maafisa wa afya wanasema uchunguzi unaendelea kubaini iwapo kweli mwanamke huyo ameambukizwa na  utachukua kati ya saa 12 hadi  24 ili kubaini ukweli.

Tayari tahadhari imechukulikuwa katika hospitali hiyo ya rufaa mjini Kericho, kuhakikisha kuwa mgonjwa huyo hakutani na watu wengine, na aliokutana nao kufanyiwa uchunguzi.

“Mgonjwa huyo alikuja akilalamika kuumwa kichwa, alikuwa na homa kali, akiendesha na kukosa hamu ya kula chochote,” amesema mmoja wa maafisa wa afya.

Ugonjwa wa Ebola, umeendelea kusababisha maafa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo kuanzia mwezi Agosti mwaka 2018, watu 1,400 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 2,000 wakiambukizwa.

Wiki iliyopita, maambukizi ya Ebola yaliripotiwa katika Wilaya ya Kasese, Magharibi mwa Uganda baada ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano aliyekuwa ametokea nchini DRC kupoteza maisha.

Kenya haijawahi kuripoti kisa hata kimoja  cha Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.