rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania John Pombe Magufuli EAC Felix Tshisekedi

Imechapishwa • Imehaririwa

Tanzania kuunga mkono ombi la DRC kujiunga jumuiya ya Afrika mashariki

media
Rais wa Tanzania, John Magufuli The New Times/Rwanda

Serikali ya Tanzania imesema itaunga mkono ombi la nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika mashariki.


Kauli hiyo imetolewa na rais wa Tanzania, John  Magufuli wakati wa hitimisho la ziara ya siku mbili ya rais wa DRC Felix Tshisekedi.

Rais Magufuli amesema atapigia chapuo ombi la DRC baada ya kuombwa na rais Tshisekedi ambay amefanya ziara ya kwanza tanzania tangu alipochaguliwa kuwa rais januari mwaka huu.

Juni 8 mwaka huu, Rais Tshisekedi aliwasilisha ombi rasmi kwa mwenyekiti wa sasa wa jumuiya hiyo Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Kwa sasa jumuiya ya Afrika mashariki inaundwa na na mataifa sita ambayo ni Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Sudan Kusini na Tanzania.