Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA

Kenya yafunga mpaka wake na Somalia kwenye eneo la Lamu

Nchi ya Kenya imetangaza kufunga mpaka wake na nchi ya Somalia wa Lamu, kwa kile Serikali imesema ni sababu za kiusalama wakati huu mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Al-Shabaab yakizongezeka.

Kisiwa cha Lamu pwani ya Kenya.
Kisiwa cha Lamu pwani ya Kenya. Erik Hersman/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Kamishna wa polisi kwenye kaunti ya Lamu Muchangi Kioi amesema mpaka huo sasa utakuwa ukifunguliwa kwaajili ya vikosi vya usalama peke yake.

Uongozi wa kaunti hiyo pia umezuia wananchi wanaoishi jirani na mpaka huo kutovuka kwenda kufanya biashara, Kioi akisema atakayekaidi atanyang'anywa leseni ya biashara na kukamatwa.

Hatua ya kufungwa kwa mpaka huu imekuja ikiwa ni wiki moja tu imepita tangu Serikali itangaze kuzuia wavuvi wake kwenda kufanya shughuli hizo kwenye pwani ya bahari na nchi ya Somalia.

Mamlaka zinasema hatua hii imekuja kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya biashara haramu zikiwemo za binadamu.

Polisi wa Lamu wanasema katika majuma kadhaa yaliyopita wamefanikiwa kukamata kilo kadhaa za sukari haramu iliyokuwa inapitishwa kwenye mpaka huo.

Eneo la Lamu limekuwa likitumiwa na wapiganaji wa Al-Shabaab kutekeleza mashambulizi na vitendo vya utekaji.

Uamuzi huu umekuja wakati ambapo nchi ya Kenya na Somalia ziko kwenye mzozo wa kidiplomasia kuhusu eneo la bahari ambalo wamekuwa wakiligombea, eneo ambalo lina hifadhi kubwa ya mafuta na gesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.