rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uchumi Kenya Uhuru Kenyatta Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Mwonekano mpya wa fedha nchini Kenya kusaidia katika vita dhidi ya ufisadi

media
Noti mpya za fedha nchini Kenya CBK

Kuchapishwa kwa noti mpya za fedha nchini Kenya, kunaelezwa kama njia mojapwapo ya kupambana na ufisadi na wizi wa fedha za umma, kauli ambayo pia imeungwa mkono na Mabalozi wa Marekani na Uingereza.


Gavana wa Benki kuu Patrick Njoroge ametangaza kuwa wale wote walio na noti ya zamani ya Shilingi 1,000 wana hadi mwezi Oktoba kuzirejesha huku wale wenye kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya Milioni wakitakiwa kujieleza ni wapi walikotoa fedha hizo.

Hata hivyo, Mbunge wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Simon Mbugua amekwenda Mahakamani kupinga matumizi ya noti hizo mpya, kwa kile anachosema katiba ilivunjwa kwa sababu Wakenya hawakuhusishwa.

Nayo Mahakama Kuu jijini Nairobi imesema kesi iliyowasilishwa na Mwanaharakati Andrew Okiya Omtata, kupinga noti hizo mpya kwa sababu zimewekwa picha ya rais wa kwanza wa taifa hilo Jomo Kenyatta, hatua ambayo ni kinyume cha katiba.

Jaji Weldon Korir amesema kuwa, suala hili ni nyeti na kuomba Jaji Mkuu David Maraga kuwateua Majaji zaidi kusikiliza kesi hiyo.

Omtata anahoji ni kwanini noti zote zina picha ya binadamu, kinyume na Katiba inayoeleza kuwa, noti zote hazistahili kuwa na picha ya mtu yeyote.