rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Somalia Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenya yapiga marufuku uvuvi katika mpaka wake na Somalia

media
Bahari Hindi AFP

Kenya imepiga marufuku shughuli za uvuvi katika Bahari ya Hindi karibu na nchi ya Somalia, kwa sababu za kiusalama.


Afisa wa serikali katika Kaunti ya Lamu, Joseph Kanyori, amesema wavuvi wote wamezuiwa kwenda kuvua katika maeneo ya Ras Kamboni na karibu na mji wa Kiunga unaopakana na nchi hizo mbili.

Kanyori ameliambia Gazeti la kila siku nchini humo la Daily Nation kuwa, hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.

Aidha, ameeleza kuwa eneo hilo la bahari limeshuhudia utekaji wa wa binadamu, dawa za kulevya pamoja na bidhaa zingine wakati huu usalama ukiimarishwa.

Marufuku haya yanakuja wakati huu Kenya na Somalia zikiwa kwenye mvutano wa kidiplomasia kuhusu mmiliki wa eneo la Bahari Hindi, linaloamiwa kuwa na utajiri wa gesi na mafuta.

Somalia imekwenda kuishtaki Kenya katika Mahakama ya Kimataifa, kulalamikia tatizo hilo la mpaka wa majini huku, ripoti zikieleza kuwa, Somalia inaungwa mkono na mataifa ya nje.

Mogadishu imetishia kumwondoa Balozi wake jijini Nairobi.