rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

Uganda Bobi Wine Yoweri Museveni

Imechapishwa • Imehaririwa

Kesi ya Bobi Wine kuanza kusikilizwa Kampala

media
Mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi, anayejulikana kwa jina la Bobi Wine akabiliwa na tuhuma za kufanya maandamano yaliyopigwa marufu kwa lengo la kuzusha machafuko.. © AFP

Mwanasiasa wa upinzani na mwanamuziki nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, anatarajiwa kufika Mahakamani jijini Kampala, ambapo mawakili wake wataomba Mahakama imwachilie huru kwa dhamana.


Bobi Wine alishtakiwa wiki iliyopita, kwa uchochezi na kuandaa maandamano yaliyopigwa marufuku mwaka uliopita jijini Kampala.

Mmoja wa wanasheria wa Bob Wine, Asuman Basalirwa anasema mteja wake amekamatwa kwa sababu za kisiasa.

Serikali kupitia naibu msemaji, Shaaban Bantaliza, imesema Bob Wine pamoja na watu wengine wanaopenda kuandamana bila kufuata sheria hawataachwa na mkono wa sheria.

Bob Wine anatajwa kuwa tishio kwa mustakabali wa siasa za rais Yoweri Kaguta Museveni.

Katika hatua nyingine, tume ya mawasiliano nchini humo imetaka kusimamishwa kazi kwa mkuu wa kitengo cha Habari cha kituo maarufu cha Televisheni cha NBS, kwa kile inachosema imekwenda kinyume na taratibu hasa kuhusu namna kituo hicho kinavyoripoti kuhusu mwanasiasa Bobi Wine.