rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Uhuru Kenyatta

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenya yaonywa kuhusu mzigo wa deni unaoikabili

media
Treni ikitumia barabara mpya ilijengwa na kampuni kutoka China, inayounganisha mji wa Pwani wa Mombasa na Nairobi. ┬ęTONY KARUMBA/AFP

Watalaam wa masuala ya Uchumi nchini Kenya pamoja na wabunge wanaionya serikali kuhusu ongezeko la deni la taifa ambalo limefikia Dola Bilioni 50.


Kuna hofu kuwa iwapo Kenya itaendelea kukopa, huenda ikakabiliwa na changamoto za kulipa, huku asilimia 70 ya deni hilo likitoka nchini China.

Kiasi kikubwa cha fedha ambazo Kenya imekopa, kimetumiwa kujenga reli ya Kati kutoka Mombasa hadi Nairobi, na sasa ujenzi mwingine unaendelea kutoka Nairobi kwenda mjini Naivasha.

Rais Uhuru Kenyatta, wiki iliyipita alifanya ziara nchini China, katika kile kinachoelezwa alienda kuomba mkopo mwingine, ili kuendeleza ujenzi wa reli hiyo hadi mjini Kisumu.