rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

Uganda Yoweri Museveni

Imechapishwa • Imehaririwa

Mahakama ya Juu nchini Uganda yafanya uamuzi wa kumwezesha rais Museveni kuwania tena

media
Rais wa Uganda Yoweri Museveni GAEL GRILHOT / AFP

Mahakama ya Juu nchini Uganda imeamua kuwa bunge lilifuata sheria wakati wa kuondoa kipengelee tata cha ukomo wa mtu anayetaka kuwania urais nchini humo, uamuzi ambao unampa nafasi rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 74, kuendelea kutafuta urais mwaka 2021.


Wakiongozwa na Jaji Mkuu Bart Katureebe, Majaji wanne walitupilia mbali kesi hiyo ya upinzani  huku Majaji watatu wakisema bunge halikufuata sheria wakati wa mabadiliko hayo.

“Kesi hii, haijakubaliwa,”amesema Jaji Mkuu Katureebe katika Mahakama ya Juu jijini Kampala.

Uamuzi huu unampa nafasi kwa rais Museveni ambaye amekuwa akiongoza nchini hiyo tangu mwaka 1986, na ana nafasi ya kuwania tena mwaka 2021 na kuendelea hadi mwaka 2026.

Mwanasheria Mkuu wa serikali Mwesigwa Rukutana amesema uamuzi huo wa Mahakama ni ushindi kwa wananchi wa Uganda.

Haya hivyo, wakili wa upinzani Erias Lukwago, amesema demokrasia ipo katika hali ngumu.

“Ni masikitiko makubwa lakini barani Afrika, ni miujiza kushinda dhidi ya serikali iliyo madarakani, aliongeza Lukwago.