Pata taarifa kuu
RWANDA-MAUAJI YA KIMBARI-JAMII

Wiki mahsusi kwa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaanza Rwanda

Rwanda imeanza kuadhimisha wiki mahsusi ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyogharimu maisha ya watu 800,000 kutoka kabila la Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani mnamo mwaka 1994.

Rais wa Rwanda Paul Kagame awacha mwenge wa kumbukumbu ya mauaji la Kigali, wakati wa maadhimisho ya mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.
Rais wa Rwanda Paul Kagame awacha mwenge wa kumbukumbu ya mauaji la Kigali, wakati wa maadhimisho ya mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda mwaka 1994. AFP/Stéphanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Ni miaka 25 tangu kutokea kwa mauaji hayo mabaya yaliyobadilisha historia ya nchi hiyo tungu uhuru wake mnamo mwaka mwizi Julai 1962 ilitawaliwa na watu kutoka kabila la Wahutu.

Kipindi hiki kinafanyika kama Umuganda, na ni juma linaloleta huzuni na matumaini kwa wakati mmoja kwa nchi ya Rwanda.

Mauaji hayo yalifanyika kote nchini humo isipokuwa wilaya moja tu.

Hiyo ni wilaya ya Giti kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Sababu ya wilaya hiyo kutoshuhudia mauaji ya kimbari ni mshikamano baina ya wananchi na uongozi uliosimama na kupinga kila aina ya uonevu.

Watutsi kwa wahutu wanamsifu aliyekuwa kiongozi wao nyakati hizo, kunyima fursa propaganda za chuki na mauaji.

Aliyekuwa kiongozi wa wilaya hiyo ya zamani ya Giti wakati wa mauaji ya kimbari ni Sebushumba Edouard, sasa ni mzee aliyestaafu.

Mwaka 1996 kiongozi huyo mstaafu alikuwa miongoni mwa wengine wengi waliotunukiwa medali za heshima kutokana na juhudi zao za kulinda raia wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi.

Katika siku miamoja mnamo mwaka 1994, watu 800,000 waliuawa kinyama nchini Rwanda. Mauji hayo yalifanywa na wahutu wenye msimamo mkali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.