rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Maswala ya kijamii Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenya: Kaunti zaidi ya kumi zakabiliwa na baa la njaa

media
Wanawake wa Turkana wakisubiri msaada wa chakula, Kalok Tonyang, katika wilaya ya Turkana kaskazini magharibi mwa Nairobi tarehe 9 Agosti 2011. Reuters/Kabir Dhanji

Serikali ya Kenya inasema Kaunti zaidi ya 10 nchini humo zinakabiliwa na baa la njaa kwa sababu ya ukame uliosababishwa na ukosefu wa mvua.


Wakenya zaidi wameendelea kuathirika na baa la njaa haswa katika Kaunti zilizoko maeneo yenye ukame kama vile Turkana ambapo vifo kutokana na jinamizi hilo vimeripotiwa, kwa mujibu wa mashahidi.

Hata hivyo Naibu rais William Ruto amesema, serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na hali hiyo hasa katika Kaunti ya Turkana iliyoathiriwa zaidi, na kukanusha ripoti kuwa watu tisa wamepoteza maisha kwa sababu ya njaa.

Kwa upande wake Waziri Eugene Wamalwa amesisitiza kwamba Kenya ina chakula cha kutosha ambacho kitasambazwa katika maeneo yaliyoathirika.