rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Somalia Ethiopia

Imechapishwa • Imehaririwa

Waziri Mkuu wa Ethiopia kuongoza mazungumzo ya maridhiano kati ya Kenya na Somalia

media
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na rais wa Somalia Mohammed Farmaajo wakielekea nchini Kenya kukutana na rais Uhuru Kenyatta @PMEthiopia

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed yupo jijini Nairobi nchini Kenya kuongoza mazungumzo kati ya rais Uhuru Kenya na mwenzake wa Somalia Mohamed Farmaajo kuhusu mvutano wa mmiliki wa eneo la Bahari Hindi linaloaminiwa kuwa na mafuta na gesi.


Jitihada za Waziri Mkuu Ahmed, zinakuja, baada ya hivi karibuni uhusiano kati ya Somalia na Kenya, kuonekana kuwa mbaya kuhusu eneo hilo la Bahari, ambalo pande zote zinadai ni lake.

Somalia imeishtaki Kenya katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, kutaka Majaji kuamua iwapo eneo hilo la  Bahari ni mali yake kwa mujibu wa mipaka ya Kimataifa.

Mwezi uliopita, serikali ya Kenya ilimrudisha nyumbani balozi wake nchini Somalia, baada ya Somalia kusema kuwa ilikuwa na mpango wa kupiga mnada eneo hilo lenye utajiri wa rasimali hiyo.

Mazungumzo haya yanarajiwa kumaliza mvutano unaoshuhudiwa kati ya nchi hizo jirani, na Waziri Mkuu Ahmed anatarajiwa kuwapatanisha viongozi wa nchi hizo mbili.

Kenya na Ethiopia zimetuma wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na kundi la Al Shabab lakini pia linawahifadhi wakimbizi wa nchi hiyo, suala ambalo huenda likasaidia katika mazungumzo hayo.