rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Rwanda

Imechapishwa • Imehaririwa

Mvutano kati ya Rwanda na Uganda: Uganda yaijibu Rwanda

media
KAmpala mji mkuu wa Uganda aambayo Rwanda inaishtumu kuwa inawatesa raia wake. REUTERS/James Akena/File Photo

Serikali ya Uganda kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Sam Kutesa, imeishtumu Rwanda kuzua habari za uongo kwamba inawapa hifadhi waasi wanchi hiyo kutoka kundi la RNC linaloongozwa na Jenerali muasi Kayumba Nyamwasa kwa lengo la kuhatarisha usalama wa taifa hilo.


Uganda imesema ikisisitiza kuwa haina lengo lolote la kuchochea vurugu au kuhatarisha usalama wa nchi yoyote jirani.

Mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi umeendelea kushuhudiwa, baada ya Rwanda kudai kuwa Uganda inawapa hifadhi maadui wa serikal yake, huku Uganda ikikanusha hilo.

Pia serikali ya Uganda imekanusha madai ya Rwanda kuwa inawatesa raia wake.

Wizara ya Mambo ya nje jijini Kampala, imesema madai hayo ya Rwanda hana msingi na ni ya uongo.

Mvutano huu umezuka, baada ya Rwanda kufunga mpaka wake na Uganda katika eneo la Katuna.

Kigali imekanusha kufunga mpaka wake wa Katuna na Uganda lakini pia kutuma wanajeshi wake mipakani.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda Richard Sezibera alinukuliwa akisema raia wa nchi yake wanateswa nchini Uganda, madai ambayo serikali ya Uganda imekanusha.

Serikali ya Rwanda, imewataka raia wake wanaokwenda nchini Uganda kuwa makini, kwa madai kuwa raia wake wanakamatwa na kurudishwa nyumbani kwa nguvu.