Pata taarifa kuu
KENYA-UN-USALAMA

Kenya yatangaza kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab

Kenya imeomba Umoja wa Mataifa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab. Kambi ya Dadaab ni kambi kubwa, iliyofunguliwa katika miaka ya 1990, karibu na mpaka wa Somalia.

Kambi ya Wakimbizi ya Dadaab, karibu na mpaka wa Somalia, ina wakimbizi zaidi ya 200,000.
Kambi ya Wakimbizi ya Dadaab, karibu na mpaka wa Somalia, ina wakimbizi zaidi ya 200,000. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Katika miaka ya nyuma kambi hiyo iliwahi kuwa kambi kubwa ya wakimbizi duniani na bado ina wakimbizi zaidi ya 200,000, hasa Wasomali.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya imetoa sababu za usalama.

Kenya imeomba Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) "kuhamisha wakimbizi kutoka Dadaab kwenda Somalia au katika nchi nyingine kwa wanaotafuta hifadhi".

Ombi hilo lilitolewa na Wizara ya Mambo ya Nje katika barua ya tarehe 12 Februari mwaka huu, ambayo ilikabidhiwa UNHCR. Hati ambayo RFI ilishuhudia.

Sababu iliyotolewa haieleweki, lakini serikali ya Kenya inasema kuwa "Dadaab ilitumiwa kama kambi ambako kunafanyiwa shughuli zinazohatarisha usalama wa taifa, ikiwa ni pamoja na ugaidi." Maneno haya ya serikali ya Kenya yanakuja siku chache baada ya shambulizila wanamgambo wa Kislam wa Al Shabab dhidi ya hoteli ya kifahari ya Dusit jijini Nairobi mwezi uliopita. Shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu 21.

Tangu wakati huo uchunguzi ulionyesha kuwa angalau mwanamgambo mmoja wa kundi hilo alipitia Dadaab kabla ya tukio hilo ambapo aliweza kupata msaada wa kutekeleza shambulio hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.