Pata taarifa kuu

Mgogoro wa Burundi: Benjamin Mkapa ashtumu EAC kushindwa kuunga mkono jitihada zake

Baada ya marais wa Uganda, Kenya na Tanzania kukabidhiwa majukumu na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea na mazungumzo na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, kutafuta njia ya kuondokana na mgogoro nchini Burundi, Mwezeshaji Benjamin Mkapa ameamua kujiuzulu kwenye nafasi yake ya usuluhishi.

Mwezeshaji katika mgogoro wa Burundi,rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa, aamua kujiuzulu kwenye nafasi yake ya usuluhishi.
Mwezeshaji katika mgogoro wa Burundi,rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa, aamua kujiuzulu kwenye nafasi yake ya usuluhishi. © UN Photo/JC McIlwaine
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Tanzania ameshtumu Jumuiya ya Afrika Mashariki kushindwa kuunga mkono jitihada zake za usuluhishi nchini Burundi.

Januari 31, Mwezeshaji katika mgogoro wa Burundi Benjamin Mkapa aliwasilisha ripoti ambayo ilikuwa bado ni siri kwa viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo Benjamin Mkapa amesema, "serikali na upinzani wanapaswa kuzungumza na kukubaliana kuhusu mfumo wa kisheria na taratibu zinazohitajika kufanyika kwa uchaguzi ujao.

Rais mstaafu wa Tanzania ameelezea masikitiko yake na hatua ya serikali ya Burundi kususia kikao cha mwisho cha mazungumzo na hali hiyo inaonyesha "msimamo wa muda mrefu " wa viongozi wa Burundi wa kutoshiriki katika mazungumzo baini ya Warundi, aliandika Mkapa.

Lakini hasa Benjamin Mkapa amesikitishwa kuona hakuungwa mkono vya kutosha katika jitihada zake, kwanza na Jumuiya ya Afrika Mashariki: "kutofanyika kwa mkutano wa kilele kuhusu mgogoro wa Burundi ulisababisha mimi kukosa uungwaji mkono wa jumuiya," amesema rais mstaafu wa Tanzania.

Bw Mkatapa ametoa wito wa kuepo kwa mazungumzo yatakayo washirikisha wadau wote kwa kufuatisha ajenda iliyowekwa katika mazungumzo ya awali na ameomba viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kushinikiza uungwaji mkono kwa mchakato wa uchaguzi kwa kuweka masharti kwa uchaguzi wa kuaminika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.