rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Al Shabab Ugaidi

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu zaidi ya 15 waangamia katika shambulio dhidi ya hoteli ya kifahari Nairobi

media
Vikosi vya usalama vya Kenya katika eneo la shambulio katika hoteli ya kifahari ya DusitD2 Nairobi, Januari 15, 2019. REUTERS/Baz Ratner

Watu wasiopungua 15 wameuawa katika shambulio la kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al Shabab linaloendelea katika hoteli kubwa ya kifahari ya DusitD2, katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, maafisa wa polisi ambao hawakutaja majina yao wameliambia shirika la Habari la AFP.


"Kwa sasa tuna watu 15 waliouawa katika shambulio, ikiwa ni pamoja na raia wa kigeni," amesema afisa wa kwanza wa polisi, idadi ambayo imethibitishwa na chanzo cha pili cha polisi ambacho kimekumbusha, hata hivyo, kwamba operesheni ya vikosi vya usalama "inaendelea" na kwamba polisi bado haijaweza kufikia katika baadhi ya maeneo ya jengo hilo.

Tayari kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia llimekiri kuwa limehusika na shambulio hilo linaloendelea.

Shambulizi hili, linawakumbusha wengi shambulizi la kigaidi lilitokea mwaka 2013 katika jengo la biashara la Westgate na kusababisha vifo vya watu 67.

Mwezi Aprili mwaka 2015 shambulizi lingine la kigaidi lilitokea katika Chuo Kikuu cha Garissa Mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 148, wengi wao wakiwa wanafunzi.

Kenya ilianza kushuhudia milipuko ya kigaidi kutoka kwa kundi la Al Shabab mwaka 2011, baada ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia, kupambana na kundi hilo la kigaidi ambalo linapambana na serikali ya Mogadishu.