Pata taarifa kuu
RWANDA-BURUNDI-RNC-USALAMA

Ripoti ya Umoja wa Mataifa: Burundi yasaidia Jenerali muasi wa Rwanda

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonesha kuwa Jenerali wa zamani kwenye jeshi la Rwanda (RDF) anayeishi uhamishoni, Kayumba Nyamwasa anasajili wapiganaji na kupata silaha kutoka nchi za Burundi, Uganda na DRC.

Jenerali muasi katika jeshi la Rwanda (RDF) Faustin Kayumba Nyamwasa.
Jenerali muasi katika jeshi la Rwanda (RDF) Faustin Kayumba Nyamwasa. AFP/MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo ya wataalamu ya tarehe 31 Desemba mwaka jana, imesema Jenerali Nyamwasa ambaye anaishi nchini Afrika Kusini kwa sasa, amesafiri mara kadhaa kwenda kwenye nchi za ukanda kuunda kundi jipya la uasi linalofahamika kama P5 ambalo liko chini ya kundi la waasi la Rwanda National Congress (RNC).

Kulingana na ripoti hiyo, kundi hilo jipya la waasi linaundwa na wapiganaji kutoka Burundi, waasi wa Kihutu wa FDLR na raia wa DRC kutoka jamii ya Wanyamulenge.

Hata hivyo Burundi imeonyooshea kidolea cha lawama kwenye ripoti hiyo kwa kukusanaya wapiganaji na kuwasafirisha mashariki mwa DRC katika maeneo ya Uvira

Wapiganaji wake wanadaiwa kutekeleza mashambulizi ya hivi karibuni kwenye maeneo ya mpaka wa nchi ya Rwanda.

Ripoti hiyo iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Desemba 18, 2018 inabaini kuwa Burundi inasaidia kundi la waasi wa Rwanda la Rwanda National Congress (RNC), lenye makao yake makuu katika mkoa wa Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kundi ambalo linaoongozwa na Jenerali muasi Kayumba Nyamwasa, afisa wa zamani wa ngazi ya juu wa jeshi la Rwanda (RDF) ambaye anaendesha uasi wa kupindua serikali ya Kagame.

Kulingana na ushuhuda uliotolewa na wapiganaji wa zamani kutoka kundi hilo, hata wanaharakati wa mashirika ya kiraia kutoka DRC na jeshi la DRC (FARDC), makao makuu ya kundi la waasi wa Rwanda la RNC yanapatikana katikaeneo la Bijabo katika wilaya ya Fizi, kilomita chache na mji mkuu wa Burundi, Bujumbura.

"Msajili mkuu wa wapiganaji wa kundi hilo anapewa hifadhi mjini Bujumbura, Burundi chini ya ulinzi mkali. Mtu huyo anafahamika kwa jina la Rashid, pia anafahamika kwa majina ya Sunday Charles. Yeye ndio anahusika na kusafirisha wapiganaji kutoka Bujumbura hadi Bijabo wakipitia kwenye Ziwa Tanganyika kwa kutumia boti", wapiganaji wa zamani wa RNC wamewaambia wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Ripoti hii inaonyesha kuwa wapiganaji wanatoka katika nchi za Afrika ya Kati, Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika, na hata katika ukanda wa Asia ya mashariki.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wapiganaji wengi wa zamani wanabaini kwamba walipewa silaha, risasi, buti, sare na chakula kutoka Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.