Pata taarifa kuu
RWANDA-BURUNDI-SANAA-USHIRIKIANO

Mvutano kati ya Burundi na Rwanda: Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Rwanda asitisha ziara yake Burundi

Mwanamuziki maarufu nchini Rwanda Ngabo Medard Jobert maarufu kama Meddy, amesitisha ziara yake katika nchi jirani ya Burundi kwa sababu za kiusalama.

Msanii wa Rwanda anaeishi Marekani Médard Jobert  Ngabo yuko Kigali kabla ya ziara yake katika nchi za Afrika Mashariki.
Msanii wa Rwanda anaeishi Marekani Médard Jobert Ngabo yuko Kigali kabla ya ziara yake katika nchi za Afrika Mashariki. The New Times (Rwanda)/Twitter
Matangazo ya kibiashara

Mwanamuziki huyo alitarajiwa kuwaburudisha wafuasi wa muziki wake jijini Bujumbura mwishoni mwa wiki hii, na sasa ziara hiyo kw a mujibu wa meneja wake, itafanyika wakati nwingine.

Hii imekuja, wakati huu uhusiano kati ya nchi hizi mbili umeendelea kuwa mbaya kwa sababu za kiusalama.

Serikali ya Bujumbiura inawatuhumu viongozi wa Rwanda hususani Rais Paul Kagame mwenyewe kuwa wanaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kufanya kila wawezalo ili kumuondoa madarakani Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Madai ambayo Rwanda inafutulia mbali na kusema ni mbinu za serikali ya Bujumbura za kutaka kujihusisha na mauaji ya kimbari dhidi ya wapinzani wake.

Zaidi ya raia wa Burundi 250,000 wamekimbilia nchi jirani ikiwezo Rwanda, kufuatia kuzuka kwa machafuko na mivutano ya kisiasa nchini Burundi.

Machafuko nchini Burundi yalianza mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka 2015 kufuatia hatua ya Pierre Nkurunziza ya kugombea tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu. Licha ya kutekelezwa jitihada za kimataifa kwa minajii ya kuhitimisha mgogoro wa Burundi, lakini juhudi hizo hadi sasa zimeshindwa kuzaa matunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.