Pata taarifa kuu
MSF-TANZANIA-MALARIA-WAKIMBIZI

MSF: Maambukizi ya Malaria yapungua katika kambi ya wakimbizi ya Nduta nchini Tanzania

Shirika la Kimataifa la Madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, linasema, kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria, kimepungua kwa kiasi kikubwa kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika kambi ya wakimbizi ya Nduta, Magharibi mwa Tanzania.

Mbinu ya kupambana na malaria katika kambi ya nduta
Mbinu ya kupambana na malaria katika kambi ya nduta www.msf.org
Matangazo ya kibiashara

MSF inasema hili limefanikiwa baada ya Shirika hilo kuanza kutumia mpango wa kudhibiti maambukizi hayo unaofahamiaka kama vector na kushuhudia maambukizi kushuka.

“Idadi ya wagonjwa wa Malaria imepungua kutoka wagonjwa 148,296 mwaka 2017 hadi 61, 668 mwezi Novemba mwaka 2018 katika kambi hiyo na maeneo jirani,” amesema Daktari Simon Masanja kutoka Shirika hilo.

Mpango huo unajumuisha usambazaji wa vyandarua vilivyowahi kutumika lakini vilivyo katika ubora, unyunyizaji wa dawa za kuwauwa mbu, na mayai yake lakini pia kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kujikinga na malaria na mpango huo.

MSF inasema mbinu hizi hazina madhara kwa binadamu. “ Tunanyunyiza dawa hii ukutani na maeneo mengine ambayo yanaweza kufikiwa na mbu, na baada ya miezi kadhaa wanauawa, dawa hii haina madhara,” amesema Godson Peter, Meneja anayehusika na masuala ya usafi na maji katika Shirika hilo.

Watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, bado wanasalia kuwa katika hatari kubwa ya kuendelea kusumbuliwa mara kwa mara ya malaria kutokana na afya yao kutokuwa imara.

Médecins Sans Frontières (MSF), limekuwa likitoa msaada wa kiafya nchini Tanzania, kwa miaka 25 sasa na mbali na wakimbizi, inawasaidia pia wananchi wa nchi hiyo wanaoishi katika mazingira magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.