Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-SOMALIA-USALAMA

Askari 1,000 wa Burundi kuondoka Somalia Februari 2019

Umoja wa Afrika umesema, wanajeshi 1,000 kutoka Burundi, wataondolewa katika kikosi chake cha AMISOM nchini Somalia kufikia mwisho wa mwezi Februari mwaka 2019.

Wanajeshi wa Burundi waliojiunga na kikosi cha Amisom, wakipiga doria katika wilaya ya Deynille, nchini Somalia, Novemba 18 mwaka 2011.
Wanajeshi wa Burundi waliojiunga na kikosi cha Amisom, wakipiga doria katika wilaya ya Deynille, nchini Somalia, Novemba 18 mwaka 2011. Reuters
Matangazo ya kibiashara

AU inasema, hatua ni kuhakikisha kuwa nchi zinazochangia wanajeshi nchini Somalia, zinakuwa na wanajeshi sawa.

Uamuzi huu unakuja wakati huu Burundi ikiendelea kuwa na uhusiano mbaya na Umoja wa Afrika kwa sababu ya mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

AMISOM inaundwa na wanajeshi kutoka mataifa matano yaukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambayo ni Uganda, Burundi, Ethiopia, Kenya na Djibouti.

Lengo likiwa ni kusaidia kurejesha amani nchini Somalia na kukabiliana na kundi la kigaidi la Al Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.