Pata taarifa kuu
BURUNDI-SISA-USALAMA-HAKI

Shirika la Wanasheria wasio kuwa na Mipaka lafunga milango yake Burundi

Shirika lisilo kuwa la kiserikali la Avocats sans frontières limesitisha shughuli zake nchini Burundi kufuatia sheria mpya ya nchi hiyo kuhusu masharika yasiyo kuwa ya kiserikali. 

Bujumbura, mji mkuu wa Burundi.
Bujumbura, mji mkuu wa Burundi. Wikimedia Commons/SteveRwanda
Matangazo ya kibiashara

Hili ni shirika la kwanza la kigeni nchini Burundi kuchukuwa uamuzi huo, siku chache kabla ya muda wa mwisho uliowekwa na serikali kuanza kutumika kwa vigezo vya wafanyakazi: 60% ya Wahutu na 40% ya Watutsi.

Mamlaka nchini Burundi ilichukuwa uamuzi wa kusitisha shughuli za mashirika yote ya kigeni na kupewa muda hadi Desemba 31 ili kuzingatia sheria mpya. Sheria hiyo, ambayo ilianza kutumika mwanzoni mwa mwaka 2017, inaweka udhibiti mkubwa wa fedha na gharama za utawala, pamoja na vigezo kwa wafanyakazi: 60% ya Wahutu na 40% ya Watutsi. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Avocats sans frontieres, Chantal van Cutsem, a,mbaye amaeamua kufunga milango ya shirika lake nchini Burundi, amkataa katu katu kutekeleza masharti hayo yaliyotolewa na serikali ya Bujumbura.

"Kulazimika kuondoka nchini na kuacha shughuli zilizokuwa zikiendelea kwa faida ya wananchi wa Burundi ni uamuzi mgumu, lakini tulijaribu kutathmini hali ya mambo na tunaona kuwa hakuna chaguo jingine ispokuwa tu kuondoka. Mamlaka imeomba tutekeleze mpango wa usawa wa kikabila. Kuwahimiza au kuwalazimisha watu kuzungumzia kabila zao ni tatizo na ni jambo ambalo haliendani na maadili ya kazi yetu, " amesema Chantal van Cutsem.

"Tunajiuliza maswali mengi kuhusu uhalali wa masharti haya chini ya sheria ya taifa na kimataifa na, bila shaka, tunaweza kuweka kando mambo ya kisiasa ambayo yanasababisha sera za ubaguzi wa kikabila," ameongeza Chantal van Cutsem. Nilitaka kuonyesha, labda, tofauti iliyo kuwepo wakati kulizungumziwa kuhusu usawa wa kikabila chini ya Mkataba wa amani wa Arusha [uliyofutwa Mei 2018] na ambao ulipelekea kusitishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe] Mkataba ambao uliwataka Warundi kugawana madaraka kulingana makabila yo katika taasisi za nchi.

Kutafuta usawa huu katika mashirika ya kiraia ni kutaka kukwamisha shughuli za mashirika ya kiraia, kwani kwani malengo la mashirika hayo hayahusiani na taasisi za serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.