Pata taarifa kuu
UGANDA-AFYA-EBOLA

Ebola: Uganda yaendelea na zoezi la upimaji wa Afya kwenye mpake wake na DRC

Serikali ya Uganda, imeendelea kuimarisha upimaji wa afya katika mpaka wake na DRC, kwa hofu ya kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Mpondwe, kwenye mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mpondwe, kwenye mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Photo: Gaël Grilhot / RFI
Matangazo ya kibiashara

Kipindi hiki cha shamrashamra za Krismasi mji wa Mpondwe kwenye mpaka wa nchi hizo mbili upo hatarini kwa sababu ya kutembeleana kwa watu wanaovuka mpaka.

Aidha, Uganda inahofia kuwa iwapo ghasia zitazuka baada ya Uchaguzi wa Jumapili, wakimbizi huenda wakaingia nchini humo na kuhatarisha pia usambazaji wa Ebola.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kukumbwa na ugonjwa hatari wa Ebola hasa mashariki mwa nchi hiyo, katika mkoa wa Kivu kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.