Pata taarifa kuu
RWANDA-MAUAJI YA KIMBARI

Wanyarandwa waomboleza kifo cha Shujaa wa mauaji ya kimbari

Raia wa Rwanda wanaomboleza kifo cha Zura Karuhimbi, mama aliyehatarisha maisha yake kwa kuwaficha zaidi ya watu 100 wakati wa mauaji kimbari mwaka 1994.

Zura Karuhimbi, 106, aliyewaficha Watutsi 150 wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 Rwanda.
Zura Karuhimbi, 106, aliyewaficha Watutsi 150 wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 Rwanda. Fred Mwasa/Twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, mama huyo mzee alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 93 huku wengine wakisema alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 100.

Kilichowagusa raia wa Rwanda ni kuwa, mama huyo alihakikisha kuwa, watu wengine wanakuwa salama dhidi ya waasi wa Interahamwe licha ya mume wake na watoto wake kuuliwa.

Rais Paul Kagame, aliwahi kumpa tuzo ya heshima kwa kitendo hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.