Pata taarifa kuu
RWANDA-SIASA-HAKI

Mwanasiasa wa upinzani Rwanda Diane Rwigara na mama yake waachiliwa huru

Mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Paul Kagame nchini Rwanda Diane Rwigara na mama yake wamefutiwa makosa yaliyokuwa yanawakabili. 

Diane Rwigara (wa 3 kutoka upande wa kushoto) na mama yake walishtakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.
Diane Rwigara (wa 3 kutoka upande wa kushoto) na mama yake walishtakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka. Cyril NDEGEYA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Rwanda imetangaza kwamba mashtaka dhidi yao hayana msingi wowote. Watuhumiwa hao walikuwa wanakabiliwa kifungo cha miaka 22 kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.

"Mashtaka yaliyokuwa yanawakabili hayana msingi wowote," amesema Jaji Xavier Ndahayo. Diane Rwigara na watuhumiwa wengine watano katika kesi hiyo, ikiwa ni pamoja na mama yake Adeline Rwigara, pia wameachiliwa huru.

Mahakama imebaini kwamba ukosoaji wa Diane Rwigara dhidi ya serikali, hasa katika mikutano na waandishi wa habari, haikuwa "kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi" kwa sababu ilikuwa haki yake katika uhuru wa kujieleza anayopewa na. Katiba ya Rwanda na sheria za kimataifa.

Majaji pia wamebaini kwamba upande wa mashtaka haujaonyesha kwamba Diane Rwigara alighushi anyaraka alipowasilisha fomu yake ya uchaguzi kwa tume ya uchaguzi kwa kushiriki katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017. Uamuzi wa kukataliwa kwa Diane Rwigara kuwania katika uchaguzi huo ulikosolewa na serikali za magharibi na mashirika ya haki za binadamu.

Mara baada ya mahakama kutoa uamuzi wake, umati wa watu waliokuwa walikuja kusikiliza kesi hiyo, walidhihirisha furaha yao. Kwa upande wa Diane Rwigara, amesema anaridhishwa na uamuzi wa mahakama: "Nina furaha sana, ninaridhishwa sana na uamuzi wa Mahakama. Yafuatayo? Ninaendelea na kile nilichoanza. Ninaendelea na siasa.

"Kwa mimi, hapakuwa na kesi," amesema Adeline Rwigara, mama wa Diane Rwigara. Kwa hiyo sikuwa na wasiwasi, wala wakati nilipokuwa gerezani hata wakati nilipoachiliwa huru kwa dhamana. Sijawahi kuwa na wasiwasi kwa sababu si kuwa na hatia. Iwe mimi wala binti yangu hatufanya chochote. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.