Pata taarifa kuu
RWANDA-HAKI

Rwanda yaonya wanasiasa wa Marekani juu ya kesi ya Rwigara

Rwanda imeambia wanasiasa wa Marekani, kutoingilia kesi inayomkabili mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Paul Kagame, Diane Rwigara.

Diane Rwigara mkosoaji mkubwa wa Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Diane Rwigara mkosoaji mkubwa wa Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS/Jean Bizimana
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Kigali imekuja, baada ya wanasiasa kadhaa wa Marekani kujitokeza na kumtetea Rwigara, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa rais Paul Kagame.

Rwigara na mama yake Adeline Rwigara, wanakabiliwa na mashataka uchochezi wa kisiasa na kuhubiri mgawanyiko. Uaumuzi kuhusu kesi yao, utatolewa wiki hii.

Mapema mwezi Oktoba Mahakama Kuu mjini Kigali iliamua kumuachilia huru kwa dhamana Diane Rwigara na mamake na kuamua kwamba watafuatiliwa wakiwa nje ya gereza.

Jaji wa mahakama kuu mjini Kigali alitangaza kwamba maombi yao ya dhamana yamekubaliwa lakini wakawekewa masharti ya kukabidhi Paspoti zao kwa mwendesha mashtaka. Aidha walitakiwa kutovuka mipaka ya jiji la Kigali bila kibali maalumu.

Wawili hao walikuwa kizuizini tangu mwaka jana kwa tuhuma za kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka. Walikanusha madai hayo wakisema yana misingi ya kisiasa.

Familia yake inasema matatizo yake yalianza wakati aliamua kuwania urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.