Pata taarifa kuu
UGANDA-ZIWA VICTORIA-AJALI-MAUAJI

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ajali ya boti nchini Uagnda yafikia zaidi ya 30

Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuzama kwa boti katika Ziwa Victoria nchini Uganda, Jumamosi iliyopita, imefikia zaidi ya 30, wakati huu zoezi la kutafuta miili zaidi ikiendelea.

Zoezi la kutafuta  miili katika Ziwa Victoria nchini Uganda
Zoezi la kutafuta miili katika Ziwa Victoria nchini Uganda AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Zura Ganyana amesema kuwa hadi sasa watu walionusurika ni 27 huku zaidi ya 60 wakiwa bado hawajapatikana.

Boti hiyo inaelezwa kuzama umbali wa mita 150 kutoka ufukweni na Sababu za kuzama zinaelezwa kuwa huenda ni idadi kubwa ya watu na hali mbaya ya hewa katika Ziwa hilo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesikitishwa na ajali hiyo. Ripoti za awali zinasema kuwa, boti hiyo haikuwa imesajiliwa na haikuwa na kibali maalum cha kufanya safara za maji.

Mauaji haya, yanakuja, miezi karibu miwili, baada ya watu zaidi ya 200 kupoteza maisha katka Ziwa hili nchini Tanzania.

Safari za maji katika Ziwa Victoria, zinaendelea kuwa hatari kutokana na uwezo mdogo wa kuwaokoa watu waliozama lakini pia bodi vibaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.