Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Umoja wa Afrika wajaribu kuishawishi serikali ya Burundi kushiriki katika mchakato wa amani

Ujumbe wa halamashauri ya amani na usalama kwenye shirika la Umoja wa Afrika ukiongozwa na Smaïl Chergui yu ziarani nchini Burundi tangu mwanzoni mwa wiki hii kwa wajili ya mashauriano na viongozi wa nchi hiyo.

Smaïl Chergui, Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Burundi, 19 Januari 2017.
Smaïl Chergui, Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Burundi, 19 Januari 2017. ONESPHORE NIBIGIRA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo wa Umoja wa Afrika unaoongozwa na Smail Chergui umewasili Burundi siku ya Jumatatu wiki hii na tayari umeshakuwa na mazungumzo na maafisa kadhaa wa serikali ya Bujumbura ikiwa ni pamoja na Makamu wa kwanza wa rais Gaston Sindimwo, waziri wa Burundi wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa, yule wa Ulinzi pamoja pia na yule wa Mambo ya Ndani.

Ziara hii ya ujumbe wa kiongozi wa halmashauri ya amani na usalama kwenye shirika la Umoja wa Afrika imejiri siku chache tu baada ya kufeli awamu ya tano ya mazungumzo baina ya wadau wa siasa ya Burundi huko mjini Arusha nchini Tanzania chini ya uongozi wa rais wa zamani wa Tanzania Benjamin William Mkapa ambapo serikali na washirika wake wamesusia kushiriki kwa hoja kwamba mwezi Oktoba kwa Burundi kihistoria ni mwezi wamusiba lakini ukweli ni kwamba serikali ya Burundi haitaki kuketi pamoja na wapinzani wake waliohusika na jaribio la mapinduzi mwezi Mei mwaka 2015.

Imedaiwa kuwa ziara hii ya Bw Chergui inalenga kupendekeza kwa viongozi wa Burundi utayarifu wa Umoja wa Afrika kuishindikiza Burundi katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2020 ili uwe uchaguzi wa haki tena wa kweli.

Badala yake Umoja wa Afrika umejikubalisha kuitetea Burundi kwenye Umoja wa Ulaya ili iondolewe vikwazo ilivyowekewa na umoja huo wa ulaya na ambavyo vimekuwa na athari nyingi kwenye uchumi wa nchi hiyo.

Hata hivyo Smail Chergui hadi sasa hajafanikiwa kukutana na rais wa Burundi Pierre NKURUNZIZA ambaye kwa muda mrefu anakuwa katika kijiji chake cha asili kaskazini mwa nchi hiyo, mkoani Ngozi.

Ni hivyo hata mabalozi wapya wapatao 10 walilazimika siku ya Jumanne kujielekeza kijijini humo ili kumkabidhi rais Nkurunziza barua zinazowateuwa kuwakilisha nchi zao Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.