Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-NKURUNZIZA-MAZUNGUMZO

Mazungumzo ya amani ya Burundi yaahirishwa

Shughuli za ufunguzi wa mazungumzo ya amani ya Burundi zilizokuwa zifanyike siku ya Jumatano mjini Arusha nchini Tanzania zimelazimika kusogezwa mbele ingawaje mwezeshaji wa mazungumzo hayo Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa hajaeleza sababu.

Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza
Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo taarifa za ndani zimedai kuwa rais Mkapa ametuma ujumbe wake kwa serikali ya Rais Pierre Nkurunziza kuitaka, itume wawakilishi katika mazungumzo hayo.

Awali,serikali ya Burundi iliomba kusogezwa mbele kwa mazungumzo hayo ikidai kuwa nchi hiyo iko kwenye maombolezo ya mwezi mzima wa Oktoba.

Wajumbe wa upinzani waishio nje ya Burundi wanaojumuika katika muungano Cenared pamoja na Wajumbe wa upinzani wa ndani wa muungano ya Amizero yabarundi wakiongozwa na Agathon Rwasa wapo Arusha tayari kwa mazungumzo hayo.

Mazungumzo ya amani yalianza baada jaribio la mapinduzi mwaka 2015, wakati rais Nkurunziza alipoamua kuwania urais kwa muhula wa tatu kinyume cha katiba.

Mazungumzo haya yalitarajiwa kuwa ya mwisho, kuleta amani nchini Burundi kuelekea Uchaguzi wa mwaka 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.