rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Bobi Wine

Imechapishwa • Imehaririwa

Bobi Wine aishtumu polisi kutumiwa kisiasa

media
Mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi, anayejulikana kwa jina la Bobi Wine kupitia muziki wa Pop, afanya mkutano na waandishi wa habari huko Washington, DC, Septemba 6, 2018. © AFP

Mbunge wa upinzani ambaye pia ni Mwanamuziki nchini Uganda Bobi Wine, amewashtumu Polisi kwa kuzuia tamasha aliloandaa mwishoni mwa juma hili jijini Kampala.


Polisi wanasema wameamua kusitisha tamasha hilo ambalo lilitarajiwa kufanyika katika uwanja wa Michezo wa Naambole kwa sababu, hajafanya maandalizi ya kutosha na wasimamizi wa uwanja huo.

Hata hivyo, mbunge huyo ambaye amejipatia umarufu siku za hivi karibuni, na kuoneakana kupendwa na vijana wengi nchini humo, amesema serikali inahofia ushawishi wake hasa kwa vijana.

Bobi Wine, ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kutokana na kupigwa mawe msafara wa Rais Yoweri Meseveni wakati wa kampeni ya uchaguzi mdogo.

Bobi Wine alitarajia kutumia tamasha hilo kuzindua album yake mpya inyofahamika kama Kyarenga.