UN na AU zataka mkataba wa amani Sudan Kusini kuanza kutekelezwa haraka
Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, unazitaka pande zote nchini Sudan Kusini, kuchukua hatua za makusudi kuanza kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa saini hivi karibuni.
Imechapishwa:
Jean Pierre Lacroix, kutoka katika jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa amezuru nchini humo na kusema utekelezwaji wa mkataba huo utasaidia kuimarisha usalama nchini humo.
Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi, walikubaliana kuunda serikali pamoja na kuunda jeshi moja ili kurejesha amani nchini humo. Hata hivyo, utekelezwaji unafanyika taratibu.
Aidha, ilikubaliwa kuwa Machar atarejea tena katika nafasi yake ya zamani ya kuwa Makamu wa kwanza wa rais.
Dunia inasubiri iwapo mkataba huo utatekelezwa kikamilifu kwa sababu, rais Kiir na Machar wameshindwa kutekeleza mikataba ya amani iliyopita.
Riek na Machar wamekuwa wakilaumiana kuhusu anayevunja mkataba huo wa amani na kunzisha vita mara kwa mara.
Maelfu ya watu wamepoteza maisha katika mzozo wa Sudan Kusini na wengine kuyakimbia makwao.