Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Mjadala waibuka kuhusu marekebisho ya Katiba Kenya

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema, hakuna anayeweza kuzuia kufanyika kwa kura ya maoni, kuirekebisha Katiba ya nchi hiyo.

Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga.
Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Odinga amesema baada ya miaka minane ya Katiba mpya, wakati umefika wa kuangalia upya na kuifanyia marekebisho ili kuendana na mazingira yalivyo nchini humo wakati huu.

Kumekuwa na wito wa kuifanyia marekebisho Katiba hiyo iliyopatikana mwaka 2010, ili kuwe na wadhifa wa Waziri Mkuu, kupunguza idadi ya wawakilishi wa nyadhifa za kisiasa, mabadiliko ambayo yanaangaziwa kuwa huenda yakasaidia kumaliza mizozo ya kisiasa nchini humo.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na Makamo rais William Ruto, wanapinga kuwepo kwa mabadiliko hayo.

Hivi karibuni vita vya maeneo viliibuka kati ya wanasiasa hawa wawili.

Matamshi ya Ruto kumhusu Raila Odinga yalizua hisia kali miongoni mwa viongozi wanaomuunga mkono Raila. Hii ni kufuatia matamshi ya Ruto kwamba Raila anayumbisha chama cha Jubilee.

Hata hivyo Bw Odinga alisema matamshi ya Makamo wa rais William Ruto, “anamfanyia njama ya kumfukuza ndani ya chama tawala cha Jubilee”, ni hofu aliyonayo kuhusu vita dhidi ya ufisadi. Odinga alisema ushirikiano wake na rais Uhuru Kenyatta kuhimiza umoja wa kitaifa na kupambana na ufisadi hautarudi nyuma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.