Pata taarifa kuu
BURUNDI - SIASA

Tishio la kufungiwa kwa mashirika yasiokuwa ya kiserikali Burundi

Siku chache baada ya kutangazwa kusitishwa kwa shughuli za mashirika yasiokuwa ya kiserikali nchini Burundi kwa kipindi cha miezi mitatu, waziri wa mambo ya ndani nchini humo Pascal Barandagiye amesisitiza kuhusu masharti yanayotakiwa kutekelezwa na taasisi hizo kabla ya kukubaliwa kufanyakazi nchini humo badala yake huenda yakafutwa moja kwa moja.

sehemu ya jiji la Bujumbura
sehemu ya jiji la Bujumbura © AFP/Carl de Souza
Matangazo ya kibiashara

Masharti hayo manne ni pamoja na kuwa na Mkataba wa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Nje, itifaki na wizara ambayo inasimamia sekta yao, ahadi ya kufuata kanuni za fedha, na hatimaye "mpango wa kurekebisha usawa wa kikabila kuajiri asilimia 40 na watutsi na asilimia 60 ya wahutu.

Ni hatua hii ya mwisho ambayo imeendelea kuzua utata, na mashirika yasiyo ya kiserikali yanatia mbele masuala ya kimaadili. Serikali ya Burundi imeendelea kushikilia msimamo wake hivyo imeyapa miezi mitatu kuwasilisha mahitaji haya, vinginevyo yatafutwa moja kwa moja. Bascal Barandagiye ni waziri wa mambo ya ndani nchini Burundi.

Lengo la serikali, inasema ni kuweka mambo sawa katika sekta ambayo, kulingana na Waziri Pascal Barandagiye, imekuwa ikigubikwa na makosa. Anataja mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo hayajafanya chochote chini kwa miaka, mengine hayapo kieshia, na kubwa zaidi mengine hayajatekeleza sheria yenye utata ambayo inatoa muongozo kuhusu kuwepo kwao tangu miezi 20.

Wakati huu majadiliano ambayo yameendelea kwa miezi kadhaa hayajawahi kuzaa matunda yoyote, duru kutoka jijini Bujumbura zinaeleza kuwa serikali imeamuwa kuyanyooshea mkono.

Hatuwa hiyo imekashifiwa vikali na mashirika ya kiraia nchini Burundi pamoja na muungano wa mashirika yanayo tetea haki za binadamu ambayo yanaona kuwa hatuwa hyo imekuja kudidimiza zaidi hali ya wananchi wa Burundi.

Ni miezi kadhaa tangu shirika la huduma la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa litangaze kuwepo kwa idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia asilimia 14 ambao wanahiraji msaada wa chakula, jambo ambalo limeendelea kutia hofu kutokana na hatuwa hiyo ya serikali ambayo inaweza kuzuia juhudi za kuwahudumia wanaohitaji msaada.

Wanasiasa pia nchini humo wametofautiana kuhusu hatuwa hiyo ya serikali ya Burundi huku baadhi wakiona kwamba kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia huku wengine wakiona ni sahihi kutekeleza sheria za nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.