Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Vita vya maneno kati ya Ruto na Odinga vyaibuka

Vita vya maneno kati ya Makamo wa rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga vimeibuka tena huku matamshi ya Ruto kumhusu Raila Odinga yamezua hisia kali miongoni mwa viongozi wanaomuunga mkono Raila. Hii ni kufuatia matamshi ya Ruto kwamba Raila anayumbisha chama cha Jubilee.

Makamo wa rais wa Kenya William Ruto.
Makamo wa rais wa Kenya William Ruto. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema matamshi ya Naibu rais William Ruto, anamfanyia njama ya kumfukuza ndani ya chama tawala cha Jubilee, ni hofu aliyonayo kuhusu vita dhidi ya ufisadi. Odinga amesema ushirikiano wake na rais Uhuru Kenyatta kuhimiza umoja wa kitaifa na kupambana na ufisadi hautarudi nyuma.

Raila Odinga, Kiongozi wa upinzani Kenya.
Raila Odinga, Kiongozi wa upinzani Kenya. REUTERS/Baz Ratner

Wakati huo huo wanasiasa wa ODM wamemshtumu William Ruto kuwa hana heshima kwa Raila Odinga.

Wadadisi wa siasa nchini humo wanaona kuwa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2022, huenda hatima ya uongozi wa nchi utaamuliwa na wanasiasa hao wawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.