Pata taarifa kuu
Utafiti waonyesha vita iliua watu 382,900 Sudan Kusini

Utafiti waonyesha vita viliua watu 382,900 Sudan Kusini

Utafiti mpya uliochapishwa juma hili unaonesha kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini vimesababisha vifo vya watu zaidi ya laki 3 na elfu 80, ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuliko ilivyokadiriwa awali na zaidi kuliko wale waliouawa kwenye mzozo wa Syria.

Wanawake wakiandamana Juba, Desemba 9, 2017, wakiomba vita vikomeshwe.
Wanawake wakiandamana Juba, Desemba 9, 2017, wakiomba vita vikomeshwe. STEFANIE GLINSKI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Utafiti huu uliofadhiliwa na taasisi ya amani ya Marekani, ulipima kiwango cha watu waliokufa kutokana na vita lakini pia mlipuko wa magonjwa na uhaba wa huduma bora za afya.

Sudan Kusini imeendelea kukumbwa na mikasa mbalimbali ikiwa ni pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo inadaiwa kuwa viliua watu wengi nchini humo.

Vita nchini Sudan Kusini vililipuka kufuatia malimbano ya ndani kati ya Rais Salva kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar, baada ya Rais Kiir kumtimu mamlakani mshirka wake huyo wa karibu.

Mikataba ya kusitisha mapigano ilifikiwa lakini mara kwa mara ilivunjwa kutokana na mapigano ya hapa na pale.

Lakini hivi karibuni mahasimu hao wawili walifikia mkataba wa amani na kugawana madaraka. Hatua hii huenda ikakomesha mapigano kati ya pande hizo mbili, mapigano yaiyodumu zaidi ya miaka sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.