Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Salva Kiir amteua naibu waziri mpya wa ulinzi

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemteua Jenerali Reuben Malek kuwa, naibu Waziri wa Ulinzi. Kiir pia amemfuta kazi Waziri wa Biashara na Viwanda Moses Hassan Tiel, na kumuweka Paul Mayom Akec

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kwenye picha).
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kwenye picha). REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Uteuzi huu umefanywa na rais Kiir licha ya Jenerali Malek kuwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa kutokana na madai ya kuhusika kwake na mauaji ya raia nchini humo.

Jenerali Riak, ambaye awali alikuwa naibu mkuu wa safu ya ulinzi ya vifaa katika jeshi, ataichukua wizara ya ulinzi ambao ni wadhifa wa pili kwa ukubwa kama naibu waziri.

Riak anakabiliwa na vikwazo kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa kwa uchochezi wa ukiukaji makubaliano ya amani.

Umoja wa Mataifa unasema Jenerali Malek, akiongoza kikosi cha jeshi la serikali, aliagiza kuwavamiwa raia katika jimbo la Upper Nile mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.