Pata taarifa kuu
TANZANIA-AJALI KIVUKO

Ajali ya kivuko Tanzania, miili 221 yapatikana, mazishi ya kitaifa kufanywa

Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mwishoni mwa juma lililopita katika ziwa Viktoria nchini Tanzania, imeongezeka na kufikia watu 218.

Waokoaji wakiopoa mwili wa mmoja wa abiria aliyekuwa katika kivuko cha MV Nyerere, wilayani Ukerewe nchini Tanzania, e21, 2018. REUTERS/Stringer
Waokoaji wakiopoa mwili wa mmoja wa abiria aliyekuwa katika kivuko cha MV Nyerere, wilayani Ukerewe nchini Tanzania, e21, 2018. REUTERS/Stringer REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano nchini Tanzania, Isack Kamwelwe, amesema zoezi la utafutaji miili zaidi linaendelea ikiwa ni katika hatua za mwisho kuhakikisha hakuna mtu aliyebaki kwenye kivuko hicho.

Waziri Kamwelwe amesema mpaka sasa miili ya watu 172 imetambuliwa na ndugu huku akithibitisha kuwa ni watu 42 ndio waliookolewa wakiwa hai kutokana na ajali hiyo.

Wakati zoezi la utafutaji miili zaidi likiendelea, Serikali imetangaza kufanya mazishi ya kitaifa baada ya wanafamilia waliopoteza ndugu zao kutaka wazikwe katika kaburi la pamoja.

Hapo jana waokoaji walifanikiwa kumpata akiwa hai, fundi mkuu wa kivuko cha MV Nyerere ambaye inadaiwa alijifungia katika chuma maalumu cha injini.

Katika hatua nyingine Serikali ya Tanzania imetangaza kutengenezwa kwa akaunti maalumu ya Benki ambayo itawawezesha wananchi walioguswa na tukio hili kuchangia fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kuwafariji wanafamilia waliopoteza ndugu zao.

Mwishoni mwa juma rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alitangaza siku 4 za maomboleze zitakazotamatika Jumatatu ya tarehe 24 ambapo pia bendera zimeendelea kupepea nusu mlingoti.

Serikali pia imesema itatoa shilingi laki 5 kwa kila familia ambayo ilipoteza ndugu katika ajali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.